Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ndege yenye misaada ya kiutu yawasili Bangui

Ndege yenye misaada ya kiutu yawasili Bangui

Ndege ya mizigo kwa ajili ya kutoa huduma za misaada ya kibinadamu kwa mamia ya raia walioathirika na machafuko yanayoendelea Jamhuri ya Afrika ya Kati imewasili leo Mjini Bangui ikiwa imesheheni tani 77 za huduma mbalimbali.

Kuwasili kwa ndege hiyo ya misaada kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kumekuja katika kipindi cha wiki moja tangu kuzuka machafuko makubwa yaliyosababisha mamia ya watu kupoteza maisha na wengine kwenda mtawanyikoni.

Ngede hiyo aina ya MD-11 inasambaza huduma mbalimbali ikiwemo mablanketi, madawa, mafuta ya kupak na huduma nyingine za kutakasa maji.

Mkurugenzi wa kanda wa UNICEF Manuel Fontaine amesema kuwa machafuko yaliyoibuka hivi karibuni yamawaathiri mamia ya watu ikiwemo watoto na wanawake ambao baadhi yao wamekimbilia uhamishoni.