Visa vya homa ya kirusi cha korona vyaripotiwa nchini Saudi Arabia

17 Disemba 2013

Shirika la afya duniani WHO limefahamishwa kuhusu visa viwili vya homa ya kirusi cha korona nchini Saudi Arabia

Kisa cha kwanza kinamhusu mama mwenye miaka 51 kutoka nchini Saudi Arabia  aliyeonekana kuwa na dalili za ugonjwa huo mnamo tarehe 20 mwezi Novemba mwaka huu. Mama huyo alionekana kuwa mgonjwa na baadaye akasafirishwa kwenda Riyadh kwa matibabu ambapo alilazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi.

Kisa cha pili kilimhusu mwanamke wa umri wa miaka 26 ambaye ni mhudumu wa afya mjiniRiyadhambaye alisema kuwa alimkaribia mwanamme wa umri wa miaka 37 ambaye alipatikana na ugonjwa huo .

Kote duniani kuanzia Septemba mwaka 2012 WHO imefahamishwa kuhusu visa 165 vya ugonjwa  huo vikiwemo vifo 71 ambapo WHO imezitaka nchi zote wanachama kundelea na  utafiti wao katika kukabiliana na ugonjwa huo.

Pia nchi wanachama zimetakiwa kuifahamisha WHO kuhusu visa vyovyote vya ugonjwa huo na kuhusu sababu zozote zilizosababisha kuwepo kwa maamumbuki yake.