Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yapeleka wahudumu zaidi wa dharura CAR

UNHCR yapeleka wahudumu zaidi wa dharura CAR

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, limesema linapeleka timu za ziada za wahudumu wa kibinadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, kufuatia kuzorota kwa hali huko na ripoti za watu kulazimika kuhama upya. Jason Nyakundi na taarifa kamili

(Taarifa ya Jason Nyakundi)

Kulingana na UNHCR, wahudumu hao wameanza kuwasili wiki hii, na wengine zaidi wapo njiani.Mjini Bangui, wafanyakazi wa UNHCR wanaripoti kuendelea kuwepo umilio ya risasi kufyatuliwa na hali ya taharuki. Hapo jana, walishuhudia takriban watu 40,000 ambao walilazimika kuhama tarehe 5 na 6 Disemba, na ambao walikuwa hawawezi kufikiwa kwa hadi sasa kwa sababu ya mapigano makali.

Inaaminika kuwa watu 210,000 wamelazimika kuhama makwao mjini Bangui pekee katika kipindi cha wiki mbili zilizopita. Katika hali hiyo hatarishi na uhaba wa chakula, anawake wengi na watoto wamevuka mto Oubangui na kukimbilia Zongo, katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo. Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR

Wengi wa watu wanaowasili upya wanaripoti maovu makubwa. Wametueleza pia kuwa watu wanaopiga kambi kwenye uwanja wa ndege Bangui wanapanga kuvuka mto na kujiunga nao Zongo. Kwenye uwanja wa ndege wa Bangui, tumelazimika kusitisha usambazaji wa misaada kwa sababu za kiusalamai. Tunatiwa hofu sana na kuwepo makundi yenye silaha karibu na maeneo yanayowapa hifadhi watu walohama makwao, na tumeomba vikosi vya Ufaransa kuongeza uwekaji doria katika maeneo karibu na vitu hivyo vya dharura.”

Huko Bossangoa, yapata kilomita 400 kaskazini magharibi mwa Bangui, makundi hasimu yalipora maduka na kuteketeza nyumba mwishoni mwa wiki. Eneo hilo linakaliwa kwa wingi na Waislamu.

Takriban watu 5,600 wamelazimika kuhama tangu kuanza tena mapigano kati ya waasi wa zamani wa Seleka na makundi yanayopinga Balaka wiki mbili zilizopita.