Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Brahimi asema pande za Syria tu ndio zitashiriki mashauriano

Brahimi asema pande za Syria tu ndio zitashiriki mashauriano

Baada ya tarehe ya mkutano wa pili wa kimataifa wa amani kuhusu Syria kutangazwa kuwa utafanyika tarehe 22 mwezi Januari kwenye jiji la Montreaux nchini Uswisi, hii leo mjumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za kiarabu kwenye suala hilo Lakhdar Brahimi amefafanua kile kitakachofanyika. Taarifa zaidi na George Njogopa.

(Taarifa ya GEorge)

Mkutano huo ambao umelenga kusaka amani kwa mzozo waSyriaunatazamiwa kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa ambao watabainisha bayana shabahayaoya kutanzua mzozo huo uliodumu kwa muda sasa. Wakati huo majadiliano ya kidiplomasia baina ya serikali yaSyriana wapinzani wake yanatazamiwa kuanza Januari 24 huko Geneva.

Mpatanishi wa mzozo huo Bwana Brahim amesema hakuna pande nyingi zitakazoruhusiwa kuhudhuria kwenye majadiliano hayo mbali ya pande zinazozozana nchiniSyria. Khawla Matta ni msemaji wa pande zinazohusika na upatanishi wa mzozo huo.

(Sauti ya Khawla)

“Tarehe 22 ni fursa kwa nchi zenye uhusiano, maslahi au ushawishi kwa Syria na zinazotaka kusaidia zinaweza kudhihirisha utayari wao wa kupatia suluhu mzozo wa Syria.Kuonyesha mapana na madhara ya janga hilo na kuonyesha kuwa kuna maslahi  ya dunia katika kulipatia jawabu. Ni kwamba mashauriano ni kati ya pande mbili za Syria na si baina  ya kila mtu atakayekuhusika. Bwana Brahimi angependa kuona nchi zeney maslahi au ushawishi zikiwepo angalau kusaidia mashauriano iwapo italazimika  lakini hawatakuwepo kwenye chumba cha mashauriano.”

Bi. Khawla amesema upande wa serikali na ule wa upinzani wanatarajiwa kuwasilisha orodha ya washiriki kabla  ya mwisho wa mwaka huu.