Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamanda mpya wa AMISOM ataka azimio la Baraza la Usalama litekelezwa haraka

Kamanda mpya wa AMISOM ataka azimio la Baraza la Usalama litekelezwa haraka

Kamanda mpya wa kikosi cha Afrika nchini Somalia, AMISOM Luteni Jenerali Silas Ntigurirwa kutoka Burundi ameomba kutekelezwa haraka iwezekanavyo azimio la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linaloongeza idadi ya askari wa kikosi hicho.

Amesema hayo punde baada ya kukabidhiwa jukumuhilorasmi mjiniMogadishu, huku akigusia pia ombi la usaidizi wa vifaa.

(Sauti ya Luteni Jenerali Ntigurirwa)

Luteni Jenerali Ntigurirwa anachukua wadhifa huo kutoka kwa Luteni Jenerali Andrew Guti wa Uganda aliyemaliza muda wake baada ya kuhudumu kwa miaka miwili.  AMISOM ina wanajeshi Elfu 17 kutoka mataifa matano ya Afrika ambayo niUganda,Burundi,Kenya,Sierra LeonenaDjibouti. Azimio la Baraza la Usalama limeongeza idadi hiyo hadi Elfu 22 ambayo inatarajiwa mwakani.