Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yaongeza operesheni zake za dharura Syria

WFP yaongeza operesheni zake za dharura Syria

Shirika la chakula ulimwenguni WFP limetangaza hii leo kuwa linapanua oparesheni zake za dharura za misaada ya chakula kwa watu milioni saba raia wa Syria waliohama makawao nadi mwa nchi yao na kwenye mataifa jirani.

Tathmini ya hivi majuzi inaonyesha kuwa karibu nusu ya watu walio nchini Syria hawana usalama wa chakula na karibu watu milioni 6.3 wanahitaji misaada ya chakula ya dharura yaa chakula. Tarifa zaidi na Grace Kaneiya

(Taarifa ya Grace)

Mwaka 2014 WFP ina mpango wa kulisha watu milioni 4.25 waliohama makwao ndani mwa Syria na karibu watu milioni 2.9 waliokimbilia mataifa jirani. Mratibu wa huduma za dharua wa WFP nchini Syria Muhannad Hadi anasema kuwa hii ndiyo hali mbaya zaidi ya kibinadamu kuwai kushuhudiwa kwa miongo kadhaa.

WFP inampango wa kuongeza mgao wa siku wa chakula kwa kuwa wengi wanaotaabika hawana chakula kwa lengo la kupunguza utapiamlo miongoni mwa watoto. Mpango mpya wa kutoa chakula shuleni pia utaanza nchini Syria hasa kwenye majimbo ya Aleppo, Al Aleppo , Al Hassakeh na vijiji vya mji wa Damascus ambapo shughuli za masomo zimeathika pakubwa.

WFP pia itaoa vocha za fedha kwa akina mama wajawazito na wale wanaonyonyesha . Vocha hizo zitawanufaisha watu 15,000 wakiwemo akina mama waliohama makwo kweney sehemu ambapo shughuli za ununuzi zinaendeshwa lakini ambapo wengi hawana pesa za kununua.