Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yatilia shaka kuhusu maisha ya watoto CAR

UNICEF yatilia shaka kuhusu maisha ya watoto CAR

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohisika na watoto UNICEF limesema kuwa kuongezeka kwa vitendo vya uvunjifu wa haki za watoto katika Jamhuri ya Afrika ya Kati kunatoa picha kwamba hali ya uhalibifu wa kibinadamu sasa umekaribia.

UNICEF imeeleza kuwa vitendo vya watoto kutekwa, kuuliwa na kutumikishwa ni baadhi ya mambo yanayoendelea kujitokeza nchini humo na limetaka kuchukuliwa kwa hatua zaidi.

Mkurugenzi Mkuu wa UNICEF Anthony Lake amesema kuwa mzozo wa Jamhuri ya Kati umesababisha maisha ya watoto wengi kuwa reheni. Amesema kuwa mkwamo huo umeathiri zaidi ya watoto milioni 2.3

Amesema kuwa mamia ya watoto wanauwawa kwa sababu tu ama wakristo ama waislamu jambo ambalo amelilaani vikali.