Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukosefu wa mbegu CAR watishia usalama wa chakula: FAO

Ukosefu wa mbegu CAR watishia usalama wa chakula: FAO

Wakulima katika Jamhuri ya Afrika ya Kati wanahitaji kupatiwa usaidizi wa haraka vinginevyo watakabiliwa na baa kubwa la ukosefu wa chakula haali itayoathiri mamilioni ya raia, shirika la chakula na kilimo FAO limeonya. George Njogopa na ripoti kamili

(Ripoti ya George)

Kwa mujibu wa FAO kiasi cha watu milioni 1.29 ikiwa ni zaidi ya asilimia 40 wanahitaji msaada wa haraka, kiwango ambacho ni mara mbili ukilinganishwa na kile kilichotolewa February mwaka huu. Kuna wasiwasi kuwa kiwango hicho huenda kikaongezeka maradufu mwaka ujao iwapo wakulima watashindwa kujiandaa na msimu wa kilimo. Uzalishaji wa mazao ulishuka kwa kiwango cha kusikitisha msimu huu kutokana na kushadidi kwa mapigano kwenye maeneo ya nchi hiyo. Mapigano hayo yaliyoibuka disemba mwaka 2012 katika eneo la Kaskazini Mashariki pia yamevuguga hali jumla ya ustawi wa kijamii.Akizungumzia hali ya kilimo ilivyo nchini humo. Mkurugenzi wa FAO katika kitengo cha misaada ya dharura Dominique Burgeon alisema kuwa hali ya wasiwasi inazidi kuongezeka kwani hata pengu chache zilizosalia sasa zimeanza kuliwa kutokana na ukosefu mkubwa wa chakula unaoendelea .