Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sudan Kusini yaripoti jaribio la kupindua serikali, UM wataka utulivu

Sudan Kusini yaripoti jaribio la kupindua serikali, UM wataka utulivu

Hali ya sintofahamu imekumba Sudan Kusini kuanzia Jumapili ambapo kumeripotiwa jaribio la kupindua serikali huku Umoja wa Mataifa ukitaka pande husika kusitisha chuki wakati huu wananchi wakikimbia kusaka hifadhi kwenye ofisi za ujumbe wa Umoja huo, UNMISS. Joshua Mmali na ripoti kamili.

(Ripoti ya Joshua)

Hilde Johnson Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, katika taarifa yake ameeleza hofu juu ya mapigano yaliyozuka mjini Juba jana jioni na ambayo yameendelea hadi asubuhi ya leo. Amezisihi pande zote kusitisha chuki baina yao na kujizuia kwa mashambulizi zaidi. Bi. Johnson amesema amekuwa na mazungumzo na viongozi wakuu ikiwemo wa ngazi ya juu kabisa nchini humo ili kuomba utulivu.

(Sauti ya Bi. Johnson)

 "Ni muhimu zaidi hivi sasa utulivu ulivyorejea, kwa viongozi wakuu kumtaka yeyote anayehuika na vurugu hizo ajizuie na kujiepusha na ghasia zozote. Sudan Kusini ina haki ya kuona amani na utulivu vinakuwepo. Hakuna yeyote anayetaka kurejea katika hali ya zamani ya ukosefu wa utulivu. Pia tunahitaji kuona ujumbe thabiti kutoka kwa viongozi wakuu ili kuhakikisha nchi nzima inabakia na amani.”

Wakati huo huo, mamia ya wananchi wamesaka hifadhi kwenye ofisi za ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS kwenye eneo la Jebel Kujur, wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto. UNMISS imesema ijapokuwa yenyewi si shirika la kibinadamu linachofanya kwa wajibu wa kulinda raia, wanawapatia mahitaji ya msingi ikiwemo matibabu. UNMISS imetumia fursa hiyo pia kukanusha ripoti kuwa inahifadhi watendaji muhimu wa kisiasa au kijeshi