Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Malkia Maxima ashuhudia usaidizi wa wakulima wadogo Dodoma, Tanzania

Malkia Maxima ashuhudia usaidizi wa wakulima wadogo Dodoma, Tanzania

Malkia Maxima wa Uholanzi ambaye ni Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ujumuishwaji wa mifumo ya fedha kwa maendeleo,  amehitimisha ziara yake ya kikazi nchini Tanzania ambayo pia aliambatana na viongozi waandamizi wa umoja huo akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la mpango wa chakula duniani, WFP.

Wakati wa ziara hiyo Malkia Maxima alizindua mpango wa kitaifa wa ujumuishaji wa mfumo wa fedha kwa maendeleo na kutembelea miradi ya wakulima wadogo wadogo wa zabibu mkoani Dodoma.

Kabla ya kuondoka nchini humo alikuwa na mahojiano maalum na George Njogopa kuhusu ziara hiyo ambapo alimweleza kuwa mfumo huo umeleta mabadiliko.

(Sauti ya Malkia Maxima)

“Mkoani Dodoma ilikuwa jambo zuri sana kushuhudia wilaya imekuwa ikiwekeza kweney mradi wa umwagiliaji kwa wakulima kati ya 200 na 300 ili waweze kupanda zabibu. Pia wilaya hiyo imekuwa ikiwadhamini wakulima kwenye benki ili waweze kupatiwa mikopo na waweze kuendesha kilimo wenyewe. Kwa hiyo aina hii ya msaada ni  muhimu sana kwani kwa wakulima kwenye zama hizi za mabadiliko ya tabia nchi, kilimo kinachotegemea mvua ni biashara ya mashaka, na umwagiliaji bila shaka unaleta mabadiliko.”