Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Benki ya dunia yataja miradi ya kunufaisha wakazi wa Goma huko DR Congo

Benki ya dunia yataja miradi ya kunufaisha wakazi wa Goma huko DR Congo

Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya dunia huko Jamhuri ya Kidemokrasia yaCongo, DRC Eustache Uoayoro amesema jimbo la kivu ya kaskazini litanufaika na miradi ya maendeleo ya kijamii kwa lengo la kuleta majibu ya haraka kwa matatizo ya wakazi wa jimbohilowaliokumbwa na ghasia za mara kwa mara.

Bwana Uaoyoro amemweleza Sifa Maguru wa Radio washirika Okapi kutoka DR Congo kuwa miradi hiyo Kumi na Mitano yenye thamani ya dola Milioni Tatu ni kwa wakazi wa vitongoji vya Rutchuru, Nyiragongo na mji wa Goma.

(Sauti  ya Oaoyoro)

Akiwa Goma Mkurugenzi Mkazi huyo wa Benki ya dunia nchini DR Congo, alihudhuria maandamano ya kuanzishwa rasmi kwa mpango wa usaidizi wa kiuchumi huko Bunagana, Kibumba na Goma.