Ban akaribisha kumalizika kwa mazungumzo baina ya Dr Congo na M23:

13 Disemba 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban  Ki-moon  amekkaribisha kuhitimishwa kwa majadiliano yaKampalabaina ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokasia yaCongona kundi la M23 kwa kutia saini azimio mjini Nairobi Kenya siku ya Alhamisi. Na pia kutolewa tamko la mwisho na Rais Yoweri Museveni waUgandana Rais Joyce Banda waMalawi, ambao walikuwa wenyeviti wa mkutano wa kimataifa wa maziwa makuu na jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).

Ban amesema hatua hii ni ya matumaini kuelekea kumaliza mzunguko wa machafuko ambayo yamesababisha madhila mengi kwa watu wa Jamhuri ya Kidemokrasia yaCongo. Katibu Mkuu ameipongeza serikali yaUgandakwa kuwa mwenyeji na kuwezesha mazungumzo hayo chini ya mwamvuli wa mkutano wa kimataifa wa maziwa makuu (ICGLR).

Ban amesema matokeo ya mazungumzo yaKampalahayatoi kinga kwa waliotekeleza uhalifu wa vita, uhalifu dhidi ya ubinadamu, mauaji ya kimbari na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.  Amezitaka pande zote kuanza kutekeleza bila kuchelewa na kuheshimu majukumuyao, na kusema Umoja wa mataifa utasaidia uwezesha mchakato huo wa utekelezaji. Ban pia ameyatolea wito makundi mengine yenye silaha Jamhuri ya Kidemokrasia yaCongokuweka silaha chini na kusaka malengoyaokwa njia ya kisiasa na amani.