Tamasha lafanywa kuwakumbuka wahamiaji walokufa maji Mediterranean:IOM

13 Disemba 2013

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM ofisi ya Roma Italia pamoja na kwanya ya Roman Philharmonic Orchestra wameandaa tamasha linalofanyika usiku wa leo kwa ajili ya kuwakumbuka wahamiaji waliopoteza maisha Lampedusa katika bahari ya Mediterranian na kwingineko kwa ajili ya kusaka maisha bora.

Tamasha hilo litakalofanyika Santa Maria del Popolo Basilica litahudhuriwa pia na mkurugenzi mkuu wa IOM balozi William Lacy Swing.

Zaidi ya watu 20,000 wamekufa maji katika miongo miwili iliyopita wakijaribu kuingia nchini Italia, mwaka 2011 watu 2300 walipoteza maisha huku wengine 700 wakiaga dunia mwaka 2013 pekee. Lengo la tamashahiloni kuhakikisha kumbukumbu za waliokufa tarehe 3 na 11 Oktoba mwaka 2013 hazipotei. Katika ajali hizo watu 400 walikufa maji na wengine 150 hawajapatikana hadi leo.