MONUSCO kuinua ustawi wa raia DRC

13 Disemba 2013

Naibu Mwakilishi maalum wa ujumbe wa kuweka utulivu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, MONUSCO, Moustapha Soumaré , ambaye pia ni Mratibu Mkazi wa masuala ya kibinadamu na Mkuu wa UNDP nchini humo, amehitimisha ziara yake ya siku mbili mjini Goma hapo jana Alhamisi.

Mwishoni mwa ziara hiyo, Bwana Soumaré  amesema, ziara hiyo ya ujumbe wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa na Benki ya Dunia mjini Goma ni ishara ya kujitoa kwa Umoja wa Mataifa kuendelea kujali maslahi ya watu wa mashariki ya DRC, na kutizama namna ya kuwasaidia kwa kuinua hali yao ya maisha.

Hapa alimweleza Sifa Maguru wa Radio washirika Okapi kuhusu wanachotarajia kutimiza  katika jimbo la Kivu ya kaskazini, mashariki mwa DRC