Watu 159,000 walazimika kuhama makwao huku 600 wakiuawa kwenye Jamhuri Afrika ya Aya Kati

13 Disemba 2013

Mapigano yanayoendelea kwenye Jamhuri ya Afrika ya Kati yamewalazimu karibu watu 159,000  kuhama makwao kwenye mji mkuu Bangui huku watu 450 wakiripotiwa kuawa na wengine 160 sehemu tofauti za nchi kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu na baraza la wakimbizi la Denmark.

Kwenye uwanja wa ndege mjini Bangui kuna watu 38,000 wasio na choo wala makao ya kuwakinga kutoka kwa mvua. Hali katika eneo hilo na sehemu zingine inazidi kudorora. Watu 12,000 wako kwenye kanisa la Saint Joseph Mukassa mjini Bangui .

Hata hivyo watu kwenye eneo hilo wanahitaji kwa dharura chakula, sabuni na misaada mingine. Kati ya hao watu 460 wanahitaji huduma za matibabu wakiwemo akina mama 100 ambapo watatu kati yao wakiwa wamejifungua.

Kuna ripoti kuhusu kushambuliwa kwa raia, kuingizwa kwa watoto jeshini, dhuluma za kijinsia na kimapenzi , uporaji na kuharibiwa kwa mali. Adrian Edward ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)

Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo imewapokea karibu wakimbizi 1800 wengi  kutoka mji mkuu Bangui wakiwmo wakimbizi 1457 walio eneo la Zongo na zaidi ya 300 walio Libenge.