Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yasafirisha tani 77 za misaada kwenda Jamhuri ya Afrika ya Kati

UNICEF yasafirisha tani 77 za misaada kwenda Jamhuri ya Afrika ya Kati

Wiki moja baada ya makabiliano makali yaliyosababisha vifo vya mamia ya watu na wengine mengi kuhama makwao kwenye mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati  msaada mkubwa wa kibinadamu umewasili hii leo mjini Bangui kwa njia ya ndege ikiwa imesheheni tani 77 ya misaada kutoka kwa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa  Mataifa UNICEF. Jason Nyakundi na taarifa kamili

 (RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Ndege hiyo imesheheni mablanketi , sabuni, mitungi ya maji, madawa , matandiko , na vifaa vinavyotumiwa na wakunga,  misaada ambayo itasambazwa kwa watu 37,500.

Mkurugenzi wa UNICEF kanda ya Magharibi na Kati mwa Afrika Manuel Fontaine amesema kuwa juma  lililopita watu kadha wengi wakiwa ni wanawake na watoto  wamekimbilia usalama wao bila chochote ila nguo walizo nazo mwilini.

Fontaine amesema kuwa misaada hiyo ya dharura itawaendea watoto na familia zenye mahitaji huku madawa yakiwaendela washirika wa UNICEF ili kuwawezesha kuendelea kutoa huduma kwa wale waliojeruhiwa siku chache zilizopita. Marixie Mercado ni msemaji wa UNICEF

 (SAUTI YA MARIXIE MERCADO)