Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ingawa usalama umeanza kuimarika mvutano wa kidini unatia hofu:UM

Ingawa usalama umeanza kuimarika mvutano wa kidini unatia hofu:UM

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa inasema ingawa hali ya usalama imeanza kuimarika katika siku za karibuni katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Bangui, bado inatiwa hofu na ongezeko la mivutano miongoni mwa jamii za  kidini.

Ofisi hiyo inasema mashambulizi kati ya jamii za Wakristo na Waislamu yanaripotiwa kutokea katika maeneo mbalimbali mjini Bangui katika siku chache zilizopita na kusababisha vifo vya watu wengi. Imeongeza kuwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unatendeka kwa misingi ya kidini ikiwa ni pamoja na uporaji na uharibifu wa nyumba, huku ikiripotiwa kuchomwa kwa msikiti na mwingine kubomolewa mapema wiki hii. Ravina Shamdasani ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa

(SAUTI YA RAVINA SHAMDASANI)