Ban apokea ripoti ya uchunguzi wa matumizi ya silaha za kemikali Syria

13 Disemba 2013

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Timu ya kuchunguza madai ya matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria, leo imewasilisha ripoti ya shughuli yake ya uchunguzi kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini New York. Timu hiyo iloongozwa na Profesa Åke Sellström wa Sweden, ilishirikisha wataalam kutoka shirika la kupinga silaha za kemikali, OPCW na Shirika la Afya Duniani, WHO. Tume hiyo iliundwa na Katibu Mkuu Ban Ki-Moon, baada ya kuripotiwa matumizi ya silaha za kemikali katika mgogoro unaoendelea nchini Syria.

Akiipokea ripoti hiyo, Katibu Mkuu ameipongeza timu hiyo kwa kazi ilofanya, na kusema kuwa mengi yamefanyika tangu madai ya kwanza ya matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria mnamo mwezi Machi mwaka huu. Amesema serikali ya Syria ilikiri kuwa na silaha za kemikali, na baadaye kusaini mkataba wa kupinga silaha za kemikali.

“Tume ya uchunguzi ya pamoja ya OPCW na Umoja wa Mataifa iliundwa, na inaendelea kufuatilia mpango wa utokomezaji wa silaha za kemikali za Syria  kwa njia salama iwezekanavyo. Matumizi ya silaha za kemikali ni ukiukwaji mkubwa wa sheria ya kimataifa, na shambulio kwa ubinadamu wetu. Tunatakiwa kusalia makini ili kuhakikisha kuwa silaha hizi hatari zinatokomezwa, siyo tu ndani ya Syria, bali popote pale.”

Ripoti hiyo imechapishwa kwenye tovuti ya ofisi ya kutokomeza silaha, na pia kwenye vyombo vya habari vya kijamii. Hapo kesho mchana, Bwana Ban atalihutubia Baraza Kuu, na pia kulihutubia Baraza la Usalama Jumatatu kuhusu ripoti hiyo.