Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wa Afrika wamejizatiti kutokomeza Malaria: Dkt. Chambers

Viongozi wa Afrika wamejizatiti kutokomeza Malaria: Dkt. Chambers

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika vita dhidi ya Malaria, Ray Chambers amezungumza na waandishi wa habari mjini New York  na kusema kuwa mafaniko yaliyodhihirika barani Afrika katika kutokomeza ugonjwa huo yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na viongozi wa bara hilo kuonyesha dhahiri uongozi wao katika vita hivyo.

Chambers amesema jitihada hizo ni pamoja na kuchangia wao katika mfuko wa kimataifa Global Fund unaohusika na harakati dhidi ya Malaria. Amesema badala ya wodi za watoto kusheheni wagonjwa wa Malaria, mafanikio yaliyopatikana yatawezesha kuongeza nguvu pia kwenye harakati dhidi ya magonjwa mengine. Mjumbe huyo maalum akatolea mfano mpango wa marais wa Afrika dhidi ya Malaria, AMA.

(Sauti ya Chambers)

 

“Mapema mwezi huu tulipokea mchango wa fedha usiotarajiwa kutoka Afrika na nchi nyingine zinazoendelea.  Ushirikiano wa viongozi wa Afrika dhidi ya Malaria, AMA ambao unajumuisha marais 49 barani Afrika. Tunashuhudia viongozi wa Afrika wakibeba jukumu kubwa la kutokomeza ugonjwa huu. Tumekuwa na mafanikio makubwa. Mwelekeo unaonekana kuwa na nuru kwani kujazia Global Fund.”

Ripoti ya shirika la afya duniani, WHO kuhusu Malaria ambayo ilizunduliwa tarehe 11 mwezi  huu imeonyesha kuwa kati ya mwaka 2000 na 2012 vifo vya watoto barani Afrika kutokana na Malaria vimepungau kwa karibu asilimia 54.