Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP imetoa wito wa kumuenzi Nelson Mandela kwa kutokomeza njaa:

WFP imetoa wito wa kumuenzi Nelson Mandela kwa kutokomeza njaa:

Mkuu wa shirika la mpango wa chakula duniani (WFP) Ertharin Cousin Alhamisi ametoa wito wa kumuenzi hayati Nelson Mandela kwa kutokomeza njaa katika watu wetu.

Bi Cousin  ameyasema hayo mjini Dar Es Salaam, Tanzania wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuwawezesha wakulima wadogowadogo kupata fursa ya huduma za fedha kama akaunti za benki, kadi za benki za mikopo ya muda mfupi, akiba na bima.

Mkurugenzi huyo wa WFP amesema ujumuishwaji katika mifumo ya fedha uliozinduliwa na serikali na benk kuu ya Tanzania una umuhimu mkubwa wa kuboresha maisha ya baadhi ya watu masikini duniani.

"Tumemuenzi wiki hii watu wengi saana duniani Rais Nelson Mandela ambaye katika hotuba yake kwenye mpango wa chakula duniani miaka kadhaa iliyopita alisema kwamba , njaa ni suala la kimaadili, kama kweli tunataka kumuenzi basi ni kwa kutokomeza njaa katika wakati wetu.Na ni nyenzo kama hii hapa Tanzania itatupa uwezo kwa kutoa msaada kwa wale wanaotutegemea kuili kubadilisha maisha yao.”

Ertharin Cousin amesema WFP na mashirika mengine yaliyoko Geneva yanaunga mkono mtazamo wa serikali kwa  Watanzania wote , hususani wasiojiweza na wakulima wadogowadogo walio masikini kupata huduma za fedha.