Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kujumuishwa katika mfumo wa fedha kutaongeza mafanikio kwa wakulima wadogowadogo:Malkia Maxima

Kujumuishwa katika mfumo wa fedha kutaongeza mafanikio kwa wakulima wadogowadogo:Malkia Maxima

Malkia Maxima wa Uholanzi ambaye ni mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya ujumuishwaji wa mifumo ya fedha kwa maendeleo, na mkurugenzi mkuu wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP Bi Ertharin Cousin leo wamezungumza na waandishi wa habari mjini Dar es salaam Tanzania na kusema kuwa kujumuishwa katika mifumo ya fedha kutaongeza mafanikio kwa watu masikini na hasa wakulima wadogowadogo. Mwandishi wetu waDar es salaamGeorge Njogopa alikuwepo na hii hapa taarifa yake.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA) 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika eneo la hudumaza za kifedha shirikishi ambaye pia ni Malkia wa Uholansi Maxima alisema hatua hiyo ni ya kupigiwa mfano.

Alisema makundi ya watu waliokuwa wakitupwa nje kwenye mzunguko wa fedha sasa wataanza kunufaika.

“ ningependa kuipongeza Benki Kuu na serikali ya Tanzania kwa kuzindua mpango huo wa huduma za fedha shirikishi ambao umelanga kuwafikia watu kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2016

Mpango huo ambao unafungua milango ya ushirikiano baina ya sekta za umma na zile binafsi umelenga kupanua huduma za kifedha kuanzia zile za kibenki mpaka mifumo mipya inatotumia simu na teknolojia nyingine za mawasiliano.

Akizungumzia mpango huo ambao unaungwa mkono na Umoja wa Mataifa, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Beno Ndula amesema kuwa mikakati iliyoko ni kwamaba hadi ifikapo mwaka 2016 asilimia ya 50 ya watu wazima wanaotumia huduma rasmi za kifedha watakuwa wamefikiwa.