Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lajadili amani na usalama Sahel, Afrika

Baraza la Usalama lajadili amani na usalama Sahel, Afrika

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limekutana kujadili hali ya amani na usalama katika eneo la Sahel barani Afrika, mwezi mmoja baada ya ziara ya Katibu Mkuu na rais wa Benki ya Dunia kwenye eneo hilo. Joshua Mmali ana taarifa kamili

(TAARIFA YA JOSHUA)

Mkutano wa leo wa Baraza la Usalama umehutubiwa na Katibu Mkuu, Ban Ki-Moon, rais wa Benki ya Dunia Jim Yong Kim na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu katika eneo la Sahel, Romano Prodi, ambao wote walilizuru eneo la Sahel mwezi mmoja ulopita. Katika hotuba yake, Bwana Ban amesema bado anahofia hali ya usalama katika eneo hilo, na juhudi zaidi zahitajika

“Kwenye ukanda mzima, vitendo vya kigaidi, ulanguzi wa silaha, madawa haramu na watu na aina nyingine za uhalifu wa kimataifa wa kupangwa vinatishia usalama. Ni lazima tufanye juhudi zaidi kukabiliana tatizo la chakula ambalo hulikumba eneo la Sahel. Kupiga vita umaskini, kuwawezesha wanawake, na nafasi kwa  vijana, na kuhakikisha kuwa watu wote wa Sahel wana kile wanachohitaji kujenga mustakhbali bora.”

Rais wa Benki ya Dunia Jim Yong Kim amesisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kukabiliana na changamoto za Sahel

“Ujumbe wetu leo ni dhahiri. Ulimwengu utaisaidia Sahel. Ziara yetu mwezi ulopita ilitupa picha kamili ya changamoto zinazowakabili watu na viongozi wa Sahel. Ilinipa hata imani zaidi kuwa, tukishirikiana, tunaweza kutoa suluhu za kubadilisha eneo hilo. Tunatakiwa kuleta pamoja nguvu za watu wote, hususan za wanawake, ili kujenga mustakhbali salama na maendeleo kwa ukanda huo.”

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Katika taarifa ya rais wa Baraza la Usalama, wanachama wa Baraza hilo wameelezea kuendelea kutiwa hofu na hali inayosikitisha katika ukanda wa Sahel, na kusisitiza utashi wake kukabiliana na changamoto sugu za kiusalama na kisiasa katika ukanda huo, ambazo zinahusiana kwa karibu na masuala ya kibinadamu na maendeleo, pamoja na athari za mabadiliko ya tabianchi na mazingira.

Wamelaani vikali mashambulizi ya kigaidi ya hivi karibuni katika ukanda huo, ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na ukatili dhidi ya raia, hususan wanawake na watoto, ambao unatekelezwa na magaidi na makundi yenye misimamo mikali.