Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafunzo ndani ya ajira kwa vijana ni muarobaini wa ukosefu wa ajira duniani: ILO

Mafunzo ndani ya ajira kwa vijana ni muarobaini wa ukosefu wa ajira duniani: ILO

Shirika la kazi duniani, ILO limesema ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana unaweza kupatiwa muarobaini, iwapo waajiri wataridhia kuboresha mfumo wa kuwapatia mafunzo ndani ya ajira vijana kama njia mojawapo ya kuboresha stadi zao na kuchangia katika maendeleo ya kampuni na mashirika. Jason Nyakundi na ripoti kamili.

(Taarifa ya Jason)

Hayo yameibuka kwenye warsha wiki hii iliyoandaliwa barani Ulaya na ILO kuhusu mwelekeo na uthabiti wa mafunzo ndani ya ajira kwa vijana na suluhu yake kwa ukosefu wa ajira miongoni mwa kundi hilo. ILO ikaeleza kuwa mifumo ya mafunzo ndani ya ajira kwa vijana au apprenticeship imekuwa mkombozi mathalani huko Austria asilimia 40 ya vijana wanaajiriwa punde baada ya kumaliza masomo yao baada ya kupitia mfumo huo. Benjamin Poredos, mnufaika wa mpango huo kutoka Austria anatoa ushuhuda.

(Sauti ya Benjamin Poredos,)

Lea Zanola mtaalamu wa stadi kutoka ILO anasema kile kinachopaswa kufanya kuimarisha mfumo huo.

(Sauti ya Lea)

Nchi nyingine iliyotajwa kufanya vyema mfumo huo na kupunguza tatizo la ajira kwa vijana ni Denmark.