Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juhudi za kunusuru misitu Uganda zaanza

Juhudi za kunusuru misitu Uganda zaanza

Uharibifu wa misitu nchini Uganda katika wilaya ya Hoima sasa ni dhahiri lakini hatua za kunusuru misitu zinachukuliwa mathalani kuanzishwa kwa mradi wa miaka mitatu wa utunzaji wa misitu nchini humo.

Juhudi hizi zinazofanywa na asasi za kiraia hapana shaka zinahitaji kuungwa mkono na serikali na jamii kwa ujumla ili kutimiza lengo la mileni la utunzaji wa mazingira. Basi ungana na  John Kibego wa Radio washirika Spice FM kutoka Uganda akikujuza kwa undani.

(MAKALA YA KIBEGO)