Hatua za kukabiliana na ukwepaji wa sheria nchini DRC zahitaji kuboreshwa: UM

11 Disemba 2013

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa hii leo imebaini kuwa mamlaka nchini DR Congo zimechukua hatua kuwajibisha wakiukwaji wa haki za binadamu wakati wa uchaguzi mwaka 2011,  lakini hata hivyo mengi hayajafanywa. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(TAARIFA YA JASON NYAKUNDI)

Ripoti hiyo inataka kuchukuliwa kwa hatua kuhakikisha kuwa uchaguzi ulio mbeleni umefanyika kwenye mazingira ya amani , mazingira ambayo yataheshimu haki za binadamu.

Ripoti hiyo iliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa inaonyesha vitendo vilivyotekelzwa kati ya tarehe mosi mwezi Oktoba mwaka 2011 na Januari 31 mwaka 2012 . Ripoti hiyo inasisitiza umuhimu uliopo wa kuwafikisha mbele ya sheria waliohusika kabla ya uchaguzi mwingibe kuandaliwa.

Uchaguzi wa mwezi Novemba mwaka 2012 ulikumbwa na ghasia kati ya wanachama wa vyama vya kisiasa katika kwa karibu mikoa yote ya nchi.

 Kando na ghasia zilizoendeshwa na raia dhidi ya raia wengine ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu ulindeshwa na maafisa wa usalama kote nchini.