Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukosefu wa ajira wa muda mrefu ni changamoto kwa nchi nyingi: ILO

Ukosefu wa ajira wa muda mrefu ni changamoto kwa nchi nyingi: ILO

Wale wanaotafuta ajira wanakumbwa na wakati mgumu wa kupata kazi kwa kipindi cha miezi sita  kwa mujibu wa ripoti mpya y shirika la kazi duniani ILO. Grace Kaneiya na maelezo zaidi.

 (TAARIFA YA GRACE KANEIYA)

Kipindi cha kutokuwa na kazi kwa wafanyikazi wengine kimekuwa kirefu kwa nchi zingine ikilinganishwa na mwka 2008.

Kwa mfano nchini Uhispania, Uingereza , Marekani, Serbia na Bulgaria ukosefu wa ajira kwa muda mrefu umeongezeka kwa asilimia 40 zaidi ikilinganishwa na mwaka 2008.

Miongoni mwa nchi zinazoendea hali ni tofauti ambapo wafanyikazi  hufanya kazi kadha kati ya kipindi cha ukosefu wa ajira hadi wakati wanapopata kazi kufuatia sababu kwamba wengi hujiunga kwenye kazi za vibarua.

Kwa mfano idadi ya watu wanliojiunga na kuhama ajira kati ya mwaka 2001 na 2012 mwaka 3.7 na asilimia 69 mtawalia kinyume na nchini Marekani  taifa lililo na fursa nyingi zaidi za ajira.