Harakati dhidi ya Malaria zaonyesha mafanikio makubwa: Ripoti

11 Disemba 2013

Shirika la afya duniani, WHO leo limetoa ripoti ya mwaka huu kuhusu Malaria inayoonyesha kuwa  juhudi za pamoja za kukabiliana na ugonjwa huo tangu mwaka 2000 zimezaa matunda zikiokoa maisha ya watu milioni 3.3.

Ripoti hiyo inasema vifo vitokanavyo na malaria vimepungua kwa asilimia 45 duniani huku barani afrika pekee idadi yake ikipungua kwa asilimia 49. Assumpta Massoi na maelezo kamili.

 (RIPOTI YA ASSUMPTA MASSOI)

Ripoti hiyo inasema kuwa pamoja na kuongezeka kitisho cha watu kukumbwa na katika kipindi cha mwaka 2000 na 2012 lakini hata hivyo kwa ujumla wake  mikakati iliyowekwa ya  kuzua na kukabiliana na tatizo la malaria imesaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza vifo na matatizo mengine yatokanayo ya ugonjwa wa malaria.

 Mafanikio hayo pia yamechangiwa na kile kilichoelezwa na ripoti hiyo kuwepo kwa utashi wa kisiasa ambapo hali hiyo pekee imepunguza tatizo la malaria kwa asilimia 29 duniani na asilimia 31 barani Afrika.

Maisha ya watu milioni 3.3 yaliokolewa katika kipindi cha mwaka 2000 na 2012 ikiwemo hata zile nchi ambazo miaka ya nyuma iliathiriwa vibaya na tatizo hilo. Kiwango hicho pia kimejumuisha kuokolewa kwa maisha ya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano ambao ndiyo wanaathiriwa zaidi na tatizo la malaria.

Hata hivyo bado kuna changamoto: Dokta Rober Newman Mkurugenzi wa mpango wa kimataifa wa malaria WHO.

(Sauti ya Dokta Newman)