Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Global Fund yazitaka serikali kuondoa vikwazo vya haki za binadamu:

Global Fund yazitaka serikali kuondoa vikwazo vya haki za binadamu:

 

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya haki za binadamu , mfuko wa kimataifa wa kupambana na ukimwi, kifua kikuu na malaria Global Fund umetoa ombi maalumu kwa la kuondoa vikwazo vyote vya haki za binadamu katika nyanja ya afya, ambavyo ni kizingiti kikubwa katika lengo la kutokomeza ukimwi, kifua kikuu na malaria.

Global Fund, imejidhatiti kulinda haki za binadamu , kueleza kwamba ubaguzi na na uhalifu vinapunguza fursa ya huduma za afya na kurejesha nyuma juhudi za kudhibiti HIV , kifua kikuu na malaria. Mfuko huo wa kimataifa unasema kuyashinda maradhi haya matatu kunahitaji kuwafikia wale wasiojiweza , wanawake na wasichana, makahaba, watu wanaotumia mihadarati, mashoga, waliobadili jinsia, wafungwa na wahamiaji.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa Global Fund, Mark Dybul, kumaliza unyanyapaa, ubaguzi na kutokuwepo uswa wa kijinsia ni kumkubali kila mtu katika familia ya kibinadamu. Akiongeza kuwa hiyo ndio njia pekee ya kuyashinda maradhi haya. Global Fund inazihimiza serikali zote na jamii kutambua na kuzungumza wazi kuhusu watu walioathirika , kuhusu usawa wa kijinsia na haki za binadamu.