MONUSCO yaanza operesheni ya kuyang’oa makundi yenye silaha DRC

10 Disemba 2013

Brigedi maalum ya kijeshi ya Ujumbe wa Kuweka Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, MONUSCO ilianza jana operesheni dhidi ya wapiganaji wa FDLR katika eneo la Kalembe, umbali wa zaidi ya kilomita mia moja kaskazini ya Goma, mashariki mwa DRC. Hayo yametangazwa Jumanne na kamanda wa majeshi ya MONUSCO, Jenerali Dos Santos Cruz katika mazungumzo ya kipekee na redio Okapi ya Umoja wa Mataifa.

(SAUTI YA SANTOS)

Jenerali Dos Santos Cruz, amesema kwamba ni mpango mrefu wa operesheni za kukabiliana na makundi yenye silaha ya DRC na ya kimataifa katika eneo hilo.