Bila ushirikiano kutoka kwa serikali hatuwezi kufanya kazi ya haki za binadamu:UM

10 Disemba 2013

Chombo kikubwa huru cha mfumo wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa leo kimezitaka serikali kushirikiana nacho na kuruhusu mashirika ya haki za binadamu na watu binafsi kushirikiana na Umoja wa mataifa bila hofu ya kutishwa au ghasia.

Wito huo kutoka kwa wataalamu maalumu 72 umekuja siku ya kimataifa ya haki za binadamu ambapo mwaka huu ni wa 20 tangu azimio laViennaambalo lilipelekea kuanzishwa kwa ofisi ya kamishina mkuu wa haki za binadamu.

 Kwa miaka mingi mataifa zaidi ya 160 yametembelewa japo na mmoja wa waatalamu wa haki za binadamu , na mataifa mengine 106 yametoa mwaliko kwa wataalamu hao wa haki amesema Chaloka Beyani kwa niaba ya kundi holo lenye wajibu wa kutoa ripoti kwa baraza la haki za binadamu na kushauri nchi kutokana na hali yao ya haki za binadamu.

Ameongeza kuwa hata hivyo mataifa 30 hayajakubali ombi la ziara ya mtaalamu yeyote, jambo ambalo linaweka bayana ukqweli kwamba sio kila ombi linaweza kukubalika. Beyani ameongeza kuwa tangu mwaka 1965 wataalamu huru wa haki za binadamu wamechagiza mijadala ya kitaifa kuhusu haki za binadamu na kuzisaidia nchi kufanyia marekebisho sheria zao.