Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO na washirika wazindua mpango mpya wa kuboresha afya ya akili

WHO na washirika wazindua mpango mpya wa kuboresha afya ya akili

Mpango mpya unaojumuisha taarifa mbalimbali kuanzia zile zinazohusu afya, haki za binadamu sera na watu wenye ulemavu umezunduliwa leo na kutoa mwanga mpya wa matumani duniani. Mpango huo ambao umezinduliwa ushirikiano wa pamoja baina ya MiNDbank,na shirika la afya ulimwenguni WHO unaweka viwango vinavyopaswa kufutwa na mataifa mbalimbali duniani. George Njogopa na maelezo kamili

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Mpango huo ambao ni jitihada za WHO inayokusudia kuleta usawa ikiwa ni sehemu kukabiliana na tatizo la uvunjifu wa haki za binadamu dhidi ya watu wenye matatizo ya akili, umezinduliwa wakati muafaka wakati duniani ikiadhimisha siku ya haki za binadamu duninai.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa kitengo cha afya ya akili ndani ya WHO, Dkt. Michelle Funk, watu wenye ulemavu bado wanakabiliwa na vikwazo mbalimbali ikiwemo vile vya kunyanyaswa na kutengwa. Vitendo hivyo ambavyo vinaripotiwa kujitokeza katika mataifa yote vinawanyima fursa ya kusonga mbele watu hao wenye ulemavu.

Amesema huduma inayojulikana kwa jina la  “ huduma rafiki” imeanzishwa kama jukwaa la kuchochea mijadala, utetezi na kuibuliwa kwa tafiti mbalimbali juu ya matatizo ya afya ya akili ili hatimaye kuleta ustawi kwa watu wa jamii hiyo.

Inaelezwa kwamba huduma za kiafya zilizopo sasa kwa watu wenye matatizo ya akili hazikidhi viwango na wakati mwingine zinatoa kikwazo kwa maisha yao.

Kupitia mpango huo mpya ulioanzishwa MiNDbank itawasaidia watunga sera kutafuta majawabu juu ya changamoto zilizopo sasa na wakati huo huo kuweka mikakati mipya itayosaidia kuumarisha ustawi wa watu wenye matatizo ya akili.