Wakati Mandela akipumzika kwa amani ni wakati wa kumuenzi kwa vitendo:Ban

10 Disemba 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon ameungana na mamilioni ya watu wa Afrika ya Kusini, familia ya Marehemu Nelson Mandela, viongozi mbalimbali , watu mashuhuri na dunia kwa ujumla kutoa heshimazake za mwisho kwa jabali la Afrika na mtetezi wa haki duniani mzee Madiba, Nelson Mandela. Assumpta Massoi na taarifa kamili

(MUSIC)

Hivyo ndivyo shamrashamra zilizoghubikwa na majonzi na furaha ya kumuenzi Nelson Mandelea aliyefariki dunia siku tano zilizopita. Familia yake, viongozi mbalimbali wa dunia akiwemo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon wamezungumza kumuhusu mpigania haki huyo ambaye ni mafano wa kuigwa duniani na jinsi atakavyokumbukwa

(SAUTI YA BAN KI-MOON-1)

Afrika ya Kusini imempoteza baba, dunia imempoteza rafiki na mshauri. Nelson Mandela alikuwa zaidi ya kiongozi shupavu wa wakati wetu huu. Alikuwa mmoja kati ya waalimu bora na alifundisha kwa kuwa mfano. Alijitolea saana na alikuwa tayari kupoteza kila kitu kwa ajili ya uhuru, usawa, demokrasia na haki."

Ban hakuishia hapo akasema sasa umewadia wakati wa kuvaa viatu vyake kwa vitendo

(SAUTI YA BAN KI-MOON-2)

Nelson Mandela sasa anapumzika, safari yake imekamilika Sasa kilichosalia ni kuongozwa na kuchagizwa na hamasa miongoni mwetu, umaarufu wa haki za binadamu na nguzo ya matumaini”

Madiba anatarajia kuzikwa Jumapili Desemba 15 kijijini alikozaliwa huko mkoa wa Cape Mashariki.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter