Watu wanaokimbia ghasia Jamhuri ya Afrika ya Kati wanahitaji misaada ya dharura:IOM

10 Disemba 2013

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linatoa huduma za dharura kwa wale walioathiriwa na mapigano kwenye Jamhuri ya Afrika ambapo mapigano Kati ya jamii yamevuruga nchi na kusababisha vifo vya watu 400 na wengine kuhama.

Watu wengi wanalala nje kweneye maeneo ya mji wa Bangui. Inakadiriwa kuwa watu 60,000 waliolazimika kuhama makwao wanaishi kwenye misikitini ,makanisa na kwenye uwanja wa ndege.

Ripoti zinasema kuwa makao hayo hufurika watu kila inapotimia masaa ya usiku kufuatia ujumbe kutoka kwa wafanyikazi wa IOM ambao wamefanikiwa kutoa misaada kidogo kutokana na ukosefu wa usalama.

Usalama wa waathiriwa, makao, usafi , afya na chakula ndilo chamagamoto kubwa kwa sasa.