Mahitaji ya misaada yazidi kuongezeka nchini Syria: UNHCR

10 Disemba 2013

Tangu kuanza kwa mwaka huu wa 2013 shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limewapelekea zaidi ya watu milioni tatu misaada wakiwemo wakimbizi wa ndani pamoja na wale wanaotaabika wanaohitaji usaidizi. Flora Nducha na taarifa kamili

 (RIPOTI YA FLORA NDUCHA)

Msaada wa UNHCR umewafikia wasyria wote kwenye majimbo manne huku takriban malori 250 yakitumwa kila wiki. UNHCR inasema kuwa nyingi ya huduma zake zinatolewa kwa watu waliolazimika kuhama makwao au kwenye sehemu zinazokumbwa na mizozo.

Misaada mingi inalengwa kwa  raia  kwenye maeneo ya Aleppo na vijiji vya mji wa Damascus maneo yanye watu wengi waliohama makwao. Misaada mingine imepelekwa mji wa Idlib moja ya mji iliyo vigumu kufikiwa na Haman ambapo ukosefu wa usalama umezuia huduma za UNHCR kati ya mwezi Mei na Novemba.

Adrian Edward ni msemaji wa UNHCR

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)

UNHCR  inasema kuwa inapatikana kwenye majimbo mengi ikiwa na jumla ya wafanyikazi 370. Kati ya misaada inayotoa ni pamoja na mablanketi , mito , mitungi ya maji na vyombo vya jikoni.