Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lamulika hali Libya na Guinea Bissau

Baraza la Usalama lamulika hali Libya na Guinea Bissau

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limekutana leo kujadili hali nchini Libya, na kutoa taarifa kuhusu hali nchini Guinea Bissau. Joshua Mmali ameufuatilia mkutano huo

(TAARIFA YA JOSHUA)

Katika taarifa ya rais wa Baraza la Usalama, baraza hilo limeelezea masikitiko yake kufuatia kuahirishwa kwa uchaguzi nchini Guinea Bissau hadi tarehe 16 Machi 2014, na hivyo kuchelewesha hatua za kurejesha uongozi wa kikatiba.

Baraza hilo limetoa wito kwa mamlaka za mpito nchini humo kuhakikisha kuwa hakuna tena kucheleweshwa au kuahirishwa tena uchaguzi huo, na hivyo kuathiri zaidi hali tete iliyopo kijamii, kiuchumi, kiusalama, kibinadamu na haki za binadamu.

Baraza hilo pia limelaani vikali mtafaruku unaoletwa mara kwa mara na wanajeshi katika masuala ya kiraia.

Katika hatua nyingine, Baraza hilo limesikiliza ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu hali nchini Libya, ikiwasilishwa na Mwakilishi Maalum na Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNSMIL, Bwana Tarik Mitri, akiangazia kwanza hali mbovu ya usalama

Vitendo vya mwezi ulopita, vimeonyesha tena haja ya mazungumzo na makundi yalojihami. Katika muktadha wa utovu wa usalama ambao umekuwepo kwa miezi mingi, UNSMIL imeomba iongezewe ulinzi wa ofisi zake”