Misitu ndiyo suluhu ya kudumu:FAO, UNECE

9 Disemba 2013

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yamezitaka nchi za Ulaya kutumia mbinu zinazochochea kuwepo kwa uchumi wa kijanii wakati zinapotekeleza miradi yake kwenye sekta ya misitu. Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula la kilimo FAO na Kamishna ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Ulaya UNECE yametoa wito huo leo wakati wa uzinduzi wa wiki ya misitu kwa nchi za Ulaya huko Rovaniemi nchini Finland. George Njogopa na taarifa kamili

(TAARIFA YA GEORGE NJOGOPA)

Mawaziri wa misitu kwa nchi za Ulaya pamoja na maafisa wengine wa ngazi za juu kutoka nchini 40 wamekutana leo nchini Finiland kwa ajili ya kujadili namna ya matumizi sahihi ya misitu ili kuziwesha nchi hizo kutimiza ndoto ya kuwa na uchumi wa kijani yaani ule unazingatia mazingira. Mwishoni mwa mkutano huo wajumbe wanatazamia kupitisha maazimio ya pamoja yatakayotumika kama dira ya kulinda na kuendeleza sekta ya misitu.

Maazimio hayo pia yatatoa mwelekeo juu ya hatua zinazopaswa kufuatwa wakati wa kuelekea kwenye kipindi cha uchumi wa kijani.Akizungumza kwenye kongamano hilo, Waziri wa misitu wa Finland Jari Koskinen……….

(Sauti ya Waziri Jari)