Uandikishaji wa mali ni wa juu zaidi kuwahi kushuhidiwa :WIPO

9 Disemba 2013

Ripoti mpya ya shirika la kimatiafa linalohuiska na kulinda mali binafsi WIPO inasema kuwa  uandikishaji wa mali mwaka 2012 ulikuwa wa juu zaidi  kuwahi kushuhudiwa.

Uandikishaji wa mali binafsi ulipungua tangu mwaka 2009 wakati wa hali ngumu ya uchumi wa dunia. Ripoti hiyo inaonyesha kuwa uandikishaji wa mali uliongezeka kwa asilimia 9.2 ambapo maombi 2.35 yalipokelewa mwaka 2012.

Awamu ya mwaka 2013 nayo inaonyesha kuwa kwa mara ya kwanza China inaongoza katika uandilkishaji wa mali kwa nembo na miundo. Francis Gurry ni Mkurugenzi Mkuu wa WIPO

"China ndiyo ofisi pekee iliyoshuhudia ongezeko maradufu la rikodi za dijitali katika sekta zote. Pili rai wa China ndiyo walioongoza kwa idadi ya mombi ya usajili, kwa raia 560,000 ikilinganishwa na Japan 480,000 na Marekani 460,000."

Gurry ameongeza kuwa baada ya hali ngumu ya uchumi ya mwaka 2009 uandikishaji wa mali binafsi umefuata mikondo tofauti. Ameongeza kusema kuwa tangu kuanza kuboreka kwa uchumi tatizo la ukosefu wa ajira halijatatuliwa.