Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mandela Akumbukwa na watu mbali mbali duniani

Mandela Akumbukwa na watu mbali mbali duniani

Mnamo Alhamisi Disemba 5 Nelson Mandela alifariki huko Afrika kusini akiwa na umri wa miaka 95. Kifo chake kimehuzunisha ulimwengu mzima kwani alikuwa  kiongozi  mashuhuri na mtetezi wa haki za bindamu ambaye alifahamika na kusifika kote ulimwenguni.

Basi katika kumbuka Mzee Mandela, ungana na Joshua Mmali kwa makala ifuatayo

Oktoba 1994. Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, akipokewa jukwaani kwenye ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Nelson Rohihlahla Mandela.

 “Mamilioni ya watu wetu wanasema ahsante, na ahsante tena, kwamba heshima ya utu wenu wenyewe kama wanadamu, iliwapa msukumo kuchukua hatua kuhakikisha kuwa utu wetu unarejeshwa pia.”

Sasa, hatunaye tena. Alhamis jioni wiki hii:

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, na habari za kifo cha Mzee Nelson Mandela.

Shujaa wa kupigania uhuru na haki, aliyetoa msukumo kwa utunzi wa nyimbo za ukombozi, mwana Afrika aliyependwa sana, na rais wa zamani wa Afrika Kusini hatimaye alitangazwa kutuaga. Habari za kifo chake ziliibua taarifa na hotuba za kumuenzi, kutoka kwa viongozi wa ngazi za juu. Kwenye Umoja wa Mataifa, Katibu mkuu Ban Ki-Moon, dakika mara tu baada ya tangazo

“Nelson Mandela alikuwa jabali wa haki na mtu wa kutoa msukumo wa utu mwenye unyenyekevu. Nelson Mandela alionyesha kinachowezekana katika dunia yetu. Cha ajabu, aliibuka kutoka miaka 27 jela bila chuki, akijizatiti kujenga Afrika Kusini kwenye misingi ya mazungumzo na maridhiano.”

Hiyo misingi ya amani na maridhiano, aliieneza hadi Afrika Mashariki, nchini Burundi, ambako alikuwa mpatanishi mkuu wa amani

Hivi sasa, Warundi wanamuenzi kwa mchango wake, kama anavyoripoti mwandishi wetu Ramadhani Kibuga

Tanzania iliwahi kumpa Mandela na wapigania uhuru wengine wa Afrika Kusini hifadhi salama, na hapa, Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowasa anamkumbuka

Je, wananchi wa kawaida Tanzania wanasema nini?

Na hawa, ni wanafunzi wavyuo

Wakubwa, kwa wadogo wanamuenzi Hayati Madiba, mtu mwenye heshima ya aina ya kipekee.