Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban na Nkurunziza wajadilia maandalizi ya uchaguzi wa Burundi wa 2015:

Ban na Nkurunziza wajadilia maandalizi ya uchaguzi wa Burundi wa 2015:

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekutana na Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza mjini Paris kandoni mwa mkutano wa Elysée unaohusu amani na usalama barani Afrika.

Viongozi hao wawili wamejadili mengi miongoni mwa hayo ni hali nchini Somalia. Ban ameishukuru serikali yaBurundikwa mchango wake mkubwa wa mchakato wa amani nchiniSomalia.

Pia wakagusia hali nzima nchini Burundi, ikiwemo maandalizi ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa mwaka 2015 na mustakhbali wa Umoja wa Mataifa kujihusisha na taifahilola maziwa makuu.