Sita kati ya watu kumi nchini Yemen watahitaji msaada:OCHA

6 Disemba 2013

Watu sita kati ya watu kumi nchini Yemen wakiwa ni watu milioni 15 kati ya watu wote milioni 25 watahitaji misaada ya kibinadamju mwaka ujao kwa mujibu wa shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA. Jason Nyakundi na maelezo kamili.

 (RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

OCHA inasema kuwa makadirio hayo yanatokana na  wito ambao utarajiwa kuzinduliwa tarehe 16 mwezi huu mjini Geneva. Mwaka huu watu milioni 13.1 walihitaji misaada. Kiasi hicho kikubwa cha watu wanaohitaji msaada sio ishara ya kuongezeka kwa mahtaji bali kuboreka kwa utafiti. Karibu nusu ya raia wote nchini Yemen , zaidi ya watu milioni  kumi hawana usalama wa chakula huku zaidi ya wasichana na wavulana milioni moja walio chini ya miaka mitano wakiwa na utapiamlo. Pia kuna zaidi ya wakimbizi wa ndani 500,000  wakiwemo pia zaidi ya wakimbizi 243,000 wengine raia wa Somalia. Yens Laerke ni msemaji wa OCHA.

(SAUTI YA YENS LAERKE)