Wanawake na watoto walengwa wakati wa uhalifu CAR

6 Disemba 2013

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yameingia na wasiwasi kufuatia kuendelea kudororo kwa hali ya usalama Jamhuri ya Afrika ya Kati na kueleza kuwa hali hiyo inaweza kukwamisha juhudi wa kuwafikia zaidi ya watu milioni 2.6 ambao wanahitaji misaada. George Njogopa na taarifa kamili.

 (TAARIFA YA GEORGE NJOGOPA)

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na watoto UNICEF limeonya juu ya kutokeza kwa machafuko makubwa hata kusababisha maafa ya kibinadamu iwapo hali inayojitokeza sasa haitadhibitiwa.

UNICEF inasema kuwa machafuko hayo yanawaathiri zaidi watoto ambao baadhi yao wanatumikishwa kama askari.

Kwa upande wake, shirika la kimataifa la mpango wa chakula, WFP, limesema kuwa shughuli za usambazaji wa chakula zimelazimika kusimamishwa kwa muda kutokana na machafuko yanayoendelea.

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeyashutumu makundi ya waasi pamoja na wapiganaji wengine kwa kuzilenga nyumba za raia na kushambulia.