Kifo cha Mzee Mandela, bendera ya UM yapepea nusu mlingoti

6 Disemba 2013

Majonzi, huzuni vimeendelea kughubika ulimwengu kufuatia kifo cha Mzee Nelson Mandela, aliyefahamika kutokana na ujasiri wake wa kupigania haki kwa maslahi ya wanaokandamizwa. Ndani ya Umoja wa Mataifa ambako misingi inayosimamiwa ya haki, amani, ulinzi na usalama Mzee Mandela aliipigania, saa Nne Asubuhi bendera za mataifa ya nchi wanachama kwenye makao makuu mjiniNew Yorkzilishushwa huku ile ya Umoja wa Mataifa ikipepea nusu mlingoti.  Kwa baraza la usalama aliyewasilisha ujumbe wa wanachama ni Balozi Gerard Araud wa Ufaransa, rais wa Barazahilokwa mwezi huu,

 (Sauti ya Balozi Araud)

 Wanachama wa Baraza la Usalama wamehuzunishwa na habari za kifo cha Nelson Mandela. Alikuwa mtu mwenye sifa ya kutoa msukumo kwa mabadiliko ya maisha ya mamilioni ya watu kote duniani. Vita vya maisha yake yote dhidi ya unyanyasaji wa ubaguzi wa rangi na mchango wake wa kipekee katika kuweka msingi wa kuibadilisha Afrika Kusini kuwa yenye umoja na demokrasia, ni mfano wa kuigwa daima kote duniani.”

Nalo baraza kuu ambalo Mzee Mandela alihutubia baada ya kutoka gerezani mwezi Septemba mwaka 1993 na hata wakati wa Urais, lilianza kikao cha leo kwa kusimama kwa dakika moja na mwakilishi wa Kudumu wa Afriak Kusini kwenye Umoja wa Mataifa Kingsley Mamabolo…

(Sauti ya Mamabolo)

Rais wa Baraza Kuu John Ashe amesema ataitisha kikao maalum cha baraza hilo kumuenzi mzee Mandela.