Kenya wasema Mzee Mandela hakuna wa kulinganishwa naye

6 Disemba 2013

Nchini Kenya Rais Uhuru Kenyatta na wananchi wake wametoa salamu kwa Taifa la Afrika Kusini, familia na wananchi kufuatia kifo cha Mzee Nelson Mandela, na hiyo ni katika salamu za rambirambi na maoni yao kama anavyoripoti mwandishi wetu wa Nairobi, Jason Nyakundi.

(Ripoti ya Jason)

Kifo cha Mzee Mandela kimegusa wengi siyo tu Afrika Kusini wala Afrika nzima bali pia ulimwengu wote. Marais mbali mbali wametuma salamu za rambirambi kwa kifo cha Mzee Mandela ambaye alisaidia nchi yake kuondoka katika minyororo ya ubaguzi. Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ni miongoni mwa marais hao na alikuwa na haya ya kusema..

 

 

Kwa niaba ya serikal na wananchi wa Kenya na kwa niaba angu binfasi napenda kutuma risala za rambirambi kwa wananchi wa Afrika Kusini, serikali, marafiki na familia ya Mzee Nelson Mandela. Nina ujumbe wa majonzi kwa Rais Jacob Zuma na mama Graca Machel. Tuko pamoja katika huzuni ya kumpoteza ambaye pengo lake haliwezi kuzibika.”

Raia waKenyawana lipi la kusema?

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter