Baraza la Usalama lasikiliza ripoti za maandalizi ya kuhitimisha majukumu ya ICTR na ICTY

6 Disemba 2013

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo mchana limesikiliza ripoti za kila baada ya miezi sita za mahakama za uhalifu wa kimbari Rwanda, ICTR na mahakama ya uhalifu ya taifa la zamani la Yugoslavia, ICTY.

Akilihutubia Baraza hilo, Rais wa Mahakama ya ICTR, Jaji Vagn Joensen amesema baada ya takriban miongo miwili ya uendeshaji mashtaka, wamefikia hatua ambapo sasa wanasubiri tu kusikiliza kesi chache za rufaa, ikitazamia kukamilisha moja mwezi huu, nne mwaka ujao, na ya mwisho moja Nyiramasuhuko, maarufu kama “Butare”, mnamo mwaka 2015.

Hata hivyo, jaji huyo amesema suala la kuwapa hifadhi uhamishoni watu walioachiwa au kutopatikana na hatia, bado linatoa utata

“Ningependa kusema, wakati ICTR inaendelea kufanya maandalizi ya kukunja jamvi la majukumu yake, suala la kuwahamisha waloachiwa kutoka Tanzania bado ni changamoto kubwa zaidi kwa ufanisi wa mahakama hii. Kwa miaka mitano ilopita, juhudi zote za kuwapa hifadhi uhamishoni watu walosalia hazijafanikiwa. Kufikia leo, watu saba waloachiwa huru na watatu walohukumiwa vifungo na kuachiwa bado wanaishi kwenye nyumba salama mjini Arusha, licha ya kwamba waliachiwa zaidi ya muongo mmoja ulopita.”

Baraza hilo pia limesikia ripoti kutoka kwa jaji wa mahakama ya uhalifu kuhusu ilokuwa Jamhuri ya Yugoslavia.