Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

AMISOM yaratibu warsha kuhusu idara za mahakama Somalia

AMISOM yaratibu warsha kuhusu idara za mahakama Somalia

Ujumbe wa muungano wa Afrika nchini Somalia AMISOM kwa ushirikiano na serikali yaSomalia na mashirika ya kiraia Alhamisi wamekamilisha warsha yenye lengo la kuboresha idara za sheria nchini humo ili kuwezesha kuhudumia masuala yanayohusina na dhuluma za kijinsia. Warsha hiyo ililenga kuhakikisha kuwa haki za wanawake zinaheshimiwa, ilihudhuriwa na wawakilishi wa serikali ya Somalia wanaofanya kazi kwenye taasisi za sheria,  AMISOM na pia mashirika ya umma. Warsha hiyo ilifunguliwa rasmi na waziri wa  masuala ya jinsi kutoka Djibouti Hasna Barkat  ambaye aliwapongeza washirika kwa kuonyesha moyo wa kuhakikisha kuwa haki za wanawake zimeheshimiwa na kulindwa.