FAO yaonya kuhusu hali ya chakula Jamhuri ya Afrika ya Kati

5 Disemba 2013

Shirika la Umoja wa Mataifa la  chakula na kilimo FAO limesema Uzalishaji wa mazao na nafaka duniani unatazamia kufikia kiwango cha juu ambacho ni karibu tani milioni 2,500 ikiwemo mpunga . FAO inaonya kuwa zaidi ya watu milioni 1.3 katika Jamhuri ya Afrika ya Kati wanahitaji msaada wa chakula kutokana na machafuko yanayoendelea. George Njogopa na ripoti kamili.

(TAARIFA YA GEORGE NJOGOPA)

 Kiwango hicho ni sawa na ongezeko la asilimia 8.4 ikilinganishwa na kile na msimu uliopita na pia kimeshinda hata kile kilichorekodiwa miaka kadhaa ya nyuma ikiwemo kile cha mwaka 2011.

Pamoja na kwamba kiwango hicho cha uzalishaji kinatazamiwa kupanda, lakini FAO imeonya kuwa hali ya usalama wa chakula barani Afrika na baadhi ya maeneo itazidi kuwa mbaya.

Hali ya mavuno msimu huu katika nchi kamaChad,Mali,Mauritania,NigernaSenegalsiyo ya kuridhisha kutokana na mabadiliko ya unyeshaji mvua. Maeneo hayo yalichelewa kupata mvua ambazo hata hivyo zilikatika mapema.

Pia huko nchiniMalishughuli za kilimo hazikufanyika vyema kutokana na mapigano yaliyosababisha maelfu ya watu kwenda mtawanyikoni.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter