Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya amani Kivu Kaskazini yaridhisha lakini hatua zaidi zahitajika: Ladsous

Hali ya amani Kivu Kaskazini yaridhisha lakini hatua zaidi zahitajika: Ladsous

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani kwenye Umoja wa Mataifa Herves Ladsous ametembelea jimbo la Kivu Kaskazini huko DR Congo na kusema kuwa hali imekuwa shwari kwenye eneo la Pinga lakini bado kuna hatua madhubuti za kuchukua kuimarisha usalama.

Radio washirika Okapi imemkariri Bwana Ladsous akisema hayo katika siku ya tatu ya ziara yake kweney eneo hilo la Pinga.

(Sauti ya Ladsous)

Katika ziara hiyo Ladsous aliambatana na viongozi kadhaa akiwemo Mkuu wa kijeshi wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani huko DR Congo, MONUSCO.