Mchango wa wanaojitolea duniani unatambulika:Ban

5 Disemba 2013

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya kujitolea , mchango wa wale wote wanaofanya hivyo kwa ajili ya amni na maendeleo ya kimataifa mchango wao unatambulika.

Hayo yamesemwa na katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kwenye ujumbe maalumu wa kuadhimish siku hii. Ameongeza kuwa leo hii watu zaidi ya biioni 1.2 duniani ambao ni vijana wenye uwezo mkubwa wa kukabili changamoto na kuwa mawkala wa mabadiliko.

Amesema kwani vijana wanapojitolea fursa hiyo inawapa ujuzi mkubwa wa maisha na kazi, pia inaboresha uwezo wao wa kuongoza na ushiriki wao katika jamii zao na jumuiya ya kimataifa kwa ujumla.

Amewashukuru vijana takriban 1000 wanaojitolea kwenye Umoja wa Mataifa katika kuchagiza amani,maendeleo endelevu na haki za binadamu.