Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wazindua kituo cha kujumuisha walemavu katika shughuli zake

UM wazindua kituo cha kujumuisha walemavu katika shughuli zake

Shughuli ya uzinduzi wa kituo jumuishi kwa walemavu kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjiniNew York, Marekani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya walemavu duniani.

Huduma zitolewazo kwenye kituo hicho kilichoandaliwa kwa usaidizi wa serikali ya Jamhuri yaKoreani pamoja na vifaa vya usaidizi wa kusikia kwa viziwi, kompyuta za kusaidia wenye uono hafifu na hata kuongeza nishati kwa baiskeli zinazotumia umeme.

Uzinduzi huo umefanywa na Katibu Mkuu wa Umoja huo Ban Ki-Moon ambaye amesema…

(Sauti ya Ban)

“Kituo hiki cha walemavu ni zaidi ya mfano wa ujumuishi. Ni mfano dhahiri tunaohitaji wa Umoja wa Mataifa katika teknolojia ya dijitali. Tunasonga mbele na suluhisho za karne ya 21 ambazo zinatumia fika ubunifu wa teknolojia. Nina imani kuwa kituo hiki kitakuwa cha mafanikio makubwa. Makao yetu makuu hapa New York yanaweza kuhamasisha uwepo wa vituo vingine kama hivi duniani.”

Rais wa Baraza Kuu John William Ashe akasema kuwa ujumuishi siyo tu kuwawezesha kuingia kwenye vyumba vya mikutano bali pia…

(Sauti ya John Ashe)

“Iwapo tunataka kujenga dunia jumuishi ni muhimu watu wenye ulemavu waweze kushiriki ipasavyo kwenye majadiliano na maazimio. Kufanya hivyo hawatakiwi tu kuingia kwenye vyumba vya mkutano bali pia wanataka taarifa katika machapisho na hata tovuti ambazo zimetengenezwa kutumika na watu wote. Kwa kupatiwa huduma hizo kituo hicho kitakuwa ni changamoto katika ujenzi wa umoja wa mataifa jumushi.”

Shukrani zilitolewa na Jenny Nilsson, Rais wa kitengo cha vijana ndani ya shirikisho la viziwi duniani ambaye alisema vijana walemavu wana mchango maalum na kuwepo kwa kituo hicho kutawawezesha kuchangia mtazamo wao kwa ajenda ya maendeleo endelevu baada ya mwaka 2015