Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IAEA yaridhika na hatua zinazochukuliwa na Japan.

IAEA yaridhika na hatua zinazochukuliwa na Japan.

Timu ya watalaalamu wa shirika la nguvu la atomiki la Umoja wa Mataifa IAEA leo wamehitimisha ukuguzi kuhusu mpango uliopewa Japan kuhusiana na mitambo yake ya uzalishaji umeme kwa kutumia mitambo ya nyuklia iliyopo Fukushima.

Timu hiyo ya wataalamu iliyoanza ukaguzi wake kuanzia Novemba 25 imepongeza Japan kutokana na namna ilivyotekeleza mapendekezo ya uboreshaji wa mitambo hiyo ambayo inatumika kuzalisha umeme.

Katika ripoti yao wataalamu hao wamesema kuwa Japan imefuata taratibu zote ikiwemo kuimarisha mifumo ya kiusalama na kuandaa kitengo maalumu kinachoshughulikia mitambo ya Fukushima.

Katika miaka ya hivi karibuni mitambo hiyo ya Fukushima ilinusurika kufumuka kufuatia mvua na tetemeko kubwa lilikoikumba Japan na kuharibu mifumo mbalimbali.